The House of Favourite Newspapers

Faiza Awaka Biashara Zake Kubuma

MSANII wa filamu Bongo, Faiza Ally amewajia juu watu wanaodai kwamba biashara yake imebuma hadi kufikia hatua ya kutupia picha ya utupu akiwa leba ili apate kiki ya kubusti biashara yake ya nguo.

 

Akizungumza na Star Mix baada ya minong’ono kusambaaa, Faiza alisema, kwa upande wake hakuna kilichobadilika kwenye maisha yake kutokana na malalamiko ya watu kwamba biashara zimekuwa ngumu wakahisi na yeye imekuwa hivyo.

 

“Sioni ugumu wowote wa biashara zangu, mambo yangu yanaenda vizuri tu, haya maisha ni kupambana na siyo kuendekeza maneno ya watu kwamba mambo yamekuwa magumu ndo ubweteke, kwanza nadhani ugumu upo kwa watu ambao siyo wachakarikaji na siyo kwa mtu kama mimi,” alisema.

Na Mayasa Mariwata

Comments are closed.