The House of Favourite Newspapers

Fatma Karume Kumrithi Tundu Lissu?

 

WAKILI wa kujitegemea, Fatma Karume, amejitosa kumrithi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), utakaofanyika Aprili 14, mwaka huu.

 

Lissu  aliteuliwa kugombea nafasi hiyo lakini ameshindwa kukidhi matakwa ya kamati kutokana na fomu ya uteuzi iliyowasilishwa kwa sekretarieti hiyo kwani kwa mujibu wa sheria mpya, kifungu cha nane cha sheria hiyo, kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa chama chochote cha siasa, kuongoza chama hicho.

 

Fatma atachuana na Godwin Mwapongo, Godfrey Wasonga na Godwin Ngwilimi,  nafasi ya makamu wa rais atagombea Rugemeleza Nshalla pekee na mgombea wa nafasi ya Mweka Hazina atakuwa ni Sadock Magai.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi wa chama hicho, Dkt. Kibuta Ongwamuhana amesema uchaguzi wa rais utatanguliwa na viongozi wa kanda utakaofanyika kila mkoa kuanzia Machi 27, mwaka huu.

 

Wakizungumzia uchaguzi huo baadhi ya mawakili wamesema wanamtabiria Fatma ushindi wa kishindo kutokana na kuwa na kaliba inayofanana na Lissu.

 

Comments are closed.