visa

FEZA AUKACHA U-TOM BOY

MTANGAZAJI wa Choice FM, Feza Kessy amefunguka kuwa ameamua kuanza kuvaa magauni na kuvaa mawigi ili kuondoa ule muonekano wa kiume (u-tom boy) kama watu wanamwambia.  Akizungumza na Gazeti la Amani, Feza amesema kwa sasa ameanza kujaribu kuvaa magauni, kuweka nywele kichwani kuona kama kuna utofauti wowote utakuja ingawa akivaa gauni na nywele wengi wanamsahau.

“Unajua kila mtu alikuwa ananiambia kwa nini navaa kama tom boy, nikaona isiwe tabu ngoja nianze kutinga gauni na niweke nywele kichwani lakini huwezi amini naona nanoga tu kwa kweli,” alisema Feza.
Toa comment