Feza Kessy, Chegge wapewa gwala
Stori: Boniphace Ngumije
DAIREKTA anayetengeneza video za viwango vya juu Bongo, Hanscana amewapa gwala wasanii wa Bongo Fleva, Feza Kessy na Chegge Chigunda kwa kuunda ‘couple’ nzuri na kutengeneza Wimbo wa Sanuka ambao kwa sasa unafanya poa.
Hanscana alisema video ya wimbo huo wa Feza ambayo audio yake imetengenezwa na Sheddy Clever kwa sasa inafanya vizuri hata kwenye televisheni za nje zenye majina makubwa na mtu akiitazama anaweza kufikiri imeshutiwa Mamtoni kumbe ni hapahapa Bongo tena Mitaa ya Sinza, jijini Dar.
“Couple ya Feza na Chegge ilikuwa ameizing kwenye ngoma ya Sanuka, kwa maoni yangu wanaweza kufanya kitu kingine kizuri ikiwa watapenda maana wameendana sana,” alisema Hanscana.



