The House of Favourite Newspapers

FULL TIME: SIMBA 0-0 YANGA,UWANJA WA TAIFA, LIGI KUU

Dk ya 90 +3: Mwamuzi anamaliza mchezo. Matokeo ni 0-0.

Dk ya 90 + 2: Simba wanafanya shambulizi kali lakini kipa wa Yanga, Kakolanya anafanya kazi nzuri ya kuokoa akishirikiana na walinzi wake.

Dk ya 90: Simba hawajakata tamaa kutafuta bao, zimeongezwa dakika 3.

Dk ya 89: Simba wanamtoa Emmanuel Okwi, anaingia Adam Salamba.

Dk ya 88: Simba wanapiga kona, inaenda kupigwa na Mohamed Ibrahim.

Dk ya 86: Ndemla anakosa nafasi ya wazi, shuti alilopiga linaenda ndivyo sivyo. Inakuwa kona.

Dk ya 83: Simba wanapata faulo karibu na kona, Zimbwe Jr anaenda kupiga faulo hiyo. Yondani anaokoa na inakuwa kona.

Dk ya 81: Kasi ya mchezo imepungua kiasi, Said Ndemla ameingia kuchukua nafasi ya Chama.

Dk ya 79: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Deus Kaseke anaingia Mrisho Ngasa.

Dk ya 78: Okwi anaumia laribu na lango la Yanga, anatibiwa kwa muda mchezo unaendelea baada ya hapo.

Dk ya 72: Makambo ameumia wakati akiwania mpira dhidi ya Pascal Wawa ambaye anapewa kadi ya njano kwa mchezo mbaya.

Dk ya 71: Simba wanafanya haraka kila wanapopata nafasi.

Dk ya 69: Kasi ya mchezo imepungua kiasi.

Dk ya 64: Simba wanashambulia kwa kasi kubwa, Kakolanya anaokoa, inakuwa kona.

Dk ya 63: Matheo anafanya shambulizi kali lakini Aishi Manula anadaka.

Simba wanamtoa Shiza Kichuya na nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Ibrahim ‘Mo’.

Dk ya 62: Kunatokea mvutano kati ya Zimbwe Jr na Dante, mwamuzi anaingilia inakuwa faulo kueleke Simba.

Dk ya 60: Kakolanya anafanya kazi nzuri, Kagere alipiga kichwa kizuri lakini kipa akautoa mpira.

Dk ya 58: Simba wanafanya shambulizi kali, Ninja wa Yanga anatoa mpira almanusura ajifunge, inakuwa kona inapigwa inaokolewa.

Dk ya 56: Tshishimbi anapata nafasi ya wazi anapiga shuti linapaa juu ya lango la Simba.

Dk ya 55: Ibrahim Ajibu ametoka, ameingia Matheo Anthony.

Dk ya 54: Kocha wa Yanga, Zahera anaonekana akimpa maelekezo Matheo ambaye anajiandaa kuingia.

Dk ya 53: Simba bado wanalishambulia lango la Yanga kwa dakika kadhaa sasa.

Dk ya 50: Shambulizi kali langoni mwa Yanga, Kapombe anaukosa mpira alipopigiwa krosi.

Dk ya 48: Simba wanafika langoni mwa Yanga lakini mpira unatoka nje.

Dk ya 46: Yanga wanafika langoni mwa Simba lakini mpira unaokolewa.

Kipindi cha pili kimeanza

Timu zinaingia uwanjani, Yanga wamekuwa wa kwanza kuingia, Simba ndiyo wanaingia baada ya Yanga na waamuzi kuingia uwanjani.

MAPUMZIKO

Dk ya 45 + 2: Mchezo unaendelea, mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza.

Dk ya 45 + 2: Kakolanya yupo chini anatibiwa baada ya kuumia, mchezo umesimama kwa muda.

Dk ya 45: Zinaonyeshwa dakika 2 za nyongeza.

Dk ya 44: Yondani anacheza faulo inapigwa kuelekea kwa Yanga, lakini walinzi wa Yanga wanaokoa.

Dk ya 40: Simba wanaongeza presha, wanafanya shambulizi kali Okwi anapiga krosi inayokoswa kutumika vizuri na Kagere.

Dk ya 39: Feisal Toto anamchezea faulo Chama, inapigwa kuelekea Yanga.

Dk ya 37: Kichuya anapiga shuti kali lakini Kakolanya anafanya kazi nzuri na kuokoa inakuwa kona ambayo inapigwa na kudakwa na Kakolanya.

Dk ya 37: Mchezo unaendelea.

Dk ya 36: Makambo anamchezea faulo Aishi Manula, mchezo unasimama akitibiwa.

Dk ya 31: Simba wanafika langoni mwa Yanga lakini wanaotea inakuwa offside.

Dk ya 28: Yanga wanapata kona.

 

Dk ya 28: Okwi anatupia wavuni lakini mwamuzi wa pembeni anasema ameotea.

Dk ya 27: Kunatokea mvutano kati ya Makambo na Wawa, Makambo anaanguka na mchezo unasimama kwa muda, lakini unaendelea baada ya mwamuzi kuwatuliza.

Dk ya 24: Chama anakosa nafasi ya wazi, shuti lake linatoka nje ya lango, waliokaa kwenye benchi la Simba walishanyanyuka kushangilia.

Dk ya 23: Beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani anapata kadi ya njano kutokana na kumchezea faulo Chama wa Simba.

Dk ya 23: Yanga wanafika langoni mwa Simba, shuti la Ibrahim Ajibu linadakwa na kipa Aishi Manula.

Dk ya 22: Simba wanakosa nafasi ya wazi kabisa, Okwi aliukosa mpira wa krosi, ukatua kwa Shiza Kichuya naye akapiga shuti kali likapaa juu ya lango.

 

Dk ya 16: Okwi anapata nafasi baada ya kumtoka Yondani, mpira unatoka nje.

Dk ya 15: Simba wanapata kona, inapigwa lakini mpira unatoka nje.

Dk ya 13: Simba wanatawala mpira kwa dakika kadhaa sasa, wanapiga pasi lakini walinzi wa Yanga wapo makini.

Dk ya 11: Simba wanafanya shambulizi kazi, Okwi anajaribu kupiga shuti lakini kipa wa Yanga, Beno Kakolanya anafanya kazi nzuri ya kuokoa.

Dk ya 8: Mohamed Hussein ambaye ni nahodha wa Simba anaingia na mpira lakini unatoka na kuwa goal kick.

Dk ya 7: Straika wa Yanga, Makambo anamchachafya Pascal Wawa na kutoa krosi lakini inashindwa kutumika vizuri. Inakuwa goal kick.

Dk ya 5: Simba wanalisogelea lango la Yanga.

Dk ya 2: Simba wanapata kona, inapigwa inaokolewa na walinzi wa Yanga.

Dk ya 1: Mchezo umeanza, Yanga wanapiga mpira unatoka unakuwa wa kurushwa kuelekea kwenye lango lao.

Mgeni Rasmi Spika wa Bunge, Job Ndugai anakagua vikosi vya timu zote mbili.

Timu zinaingia uwanjani.

Huu ni mtanange wa Simba dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ni kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

Comments are closed.