The House of Favourite Newspapers

Funga Inavyoweza Kusaidia Kupunguza Unene

0

MPENZI msomaji ni matumaini yangu unaendelea vyema na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao licha ya kuwa na faida za kiroho pia una faida kwa siha.

Leo katika makala haya nitazungumzia swaumu na siha ambayo ni maalum kwa mwezi huu mtukufu, tutajadili namna ya kupunguza uzito wakati wa kufung na tule vipi na vyakula vya aina gani ili kutodhuru tumbo. Funga ya Mwezi wa Ramadhani inaweza kuwa na faida kwa afya iwapo itatakelezwa ipasavyo.

Mwili unapokosa chakula, huyeyusha mafuta ili kutengeneza nishati. Suala hilo huweza kusababisha unene kupungua. Hata hivyo, iwapo utafunga kwa muda mrefu mwili huanza kuyeyusha protini zilizo katika misuli suala ambalo ni hatari kwa afya.

Dakta Razeen Mahroof wa Chuo Kikuu cha Oxford anasema kwamba, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya lishe na afya na kwamba Ramadhani licha ya kuwa ni fursa ya kuimarisha imani, pia inaweza kusaidia kupunguza uzito.

Mabadiliko yanayotokea mwilini wakati wa kufunga hutegemea swaumu imefungwa kwa muda gani. Kwa kawaida mwili huingia katika hali ya kufunga, saa 8 na zaidi baada ya kukosa chakula, wakati utumbo unapomaliza kufyonza virutubisho katika chakula tumboni.

Katika hali ya kawaida, chanzo cha nishati ya miili ni glukosi inayohifadhiwa kwenye ini na misuli. Wakati mtu anapofunga, chanzo hicho cha glukosi iliyohifadhiwa hutumika kwanza kudhamini nishati ya mwili, inapomalizika mafuta nayo huanza kufyonzwa na kuyeyushwa ili kutengeneza nishati.

Suala hili likitekelezwa ipaswavyo, husababisha wanaofunga kupunguza uzito na unene.

Yafuatayo ni maelekezo yanayoweza kusaidia kujua namna ya kuzuia kula sana wakati wa mwezi huu na hivyo kujiepusha kunenepa na pia kutolisababishia tumbo madhara.

Kwanza kabisa unashauriwa kujiepusha kula vyakula vyenye kalori na mafuta mengi pale unapofuturu.

Watu wengi husubiri wakonde pale wanapofunga, lakini pengine wakati wa futari na daku hula vyakula vyenye kalori nyingi kuliko siku za kawaida pale wanapokuwa hawajafunga.

JIEPUSHE HAYA

Pia inashauriwa kuwa, wakati wa kufuturu unapaswa kujiepusha kufungua kwa maji baridi, soda, juisi na vinywaji vinginevyo kama hivyo, na badala yake ni bora ufungue kwa kunywa maji ya uvuguvugu au chai.

FUNGUA KWA KULA HIVI

Pia unashauriwa kufungua swaumu yako kwa kula tende, zabibu kavu, asali au chakula chochote kitamu lakini kwa kiwango kidogo, kwani kufanya hivyo hudhibiti hamu ya kula, na kumfanya mtu asiwe na hamu ya kula sana.

Miongoni mwa vyakula vinavyofaa kula wakati wa kufuturu ni kama chai isiyokuwa na majani mengi, maziwa moto, bokoboko lisilokuwa na mafuta mengi, mkate na jibini na mboga za majani kwa maana ya vegetables.

Pia tunashauriwa kuwa pale tunapofuturu ni bora tusinywe maji mengi wakati wa kula, kwani kunywa maji pamoja na chakula husababisha utumbo kuwa na majimaji suala linalokwamisha uyeyushaji chakula.

Ni bora kunywa maji hatua kwa hatua baada ya kufuturu hadi wakati wa daku ili kuepusha kulijaza tumbo maji kwa wakati mmoja.

Wiki ijayo tutaelezea ulaji

Leave A Reply