The House of Favourite Newspapers

Gor Mahia Mabingwa SportPesa Super Cup, Waifunga Simba 2-0


TIMU ya Gor Mahia ya Kenya wametwaa ubingwa wa SportPesa Super Cup kwa mara ya pili mfululizo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba ya Tanzania.

Mabao ya Gor Mahia yamefungwa na wanasoka wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere na Jaqcues Tuyisenge.

 

Gor Mahia inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Mwingereza Dylan Kerr,  pamoja na kuzawadiwa Dola za Kimarekani 30,000 watakwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park jijini Liverpool, England.

Simba wamepewa Dola za Marekani 10,000 na Singida United waliomaliza nafasi ya tatu kwa kuifunga Kakamega Homeboyz kwa penati 5-1 baada ya sare ya 1-1,  watapatiwa Dola 7, 500 ambapo washindi wa nne watapewa Dola 5,000.

Kariobangi Sharks ya Kenya, Yanga ya Tanzania Bara na JKU ya Zanzibar kila moja zitapata dola 2,500 baada ya kutolewa hatua ya kwanza ya mashindano.

Kikosi cha Gor Mahia kilikuwa: Shaaban Odhoji, Harun Shakava, Godfrey Walusimbi, Pjilemon Otieno, Ernest Wendo, Francis Kahata, George Odhiambo/Juma dk82, Humphrey Mieno/Innocent Wafula dk67, Meddie Kagere/Bernard Omondi dk91, Jaqcues Tuyisenge/Bernard Ondiek dk93 na Joash Onyango.

Simba SC: Aishi Manula, Shomari Kapombe/Ally Shomari dk68, Erasto Nyoni, Paul Bukaba, Yussuf Mlipili/Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dk59, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Mohammed Ibrahim dk89, Muzamil Yassin, Adam Salamba, Rashid Mohammed na Rashid Juma/Marcel Kaheza dk57.

PICHA: MUSA MATEJA NAKULU KENYA-GPL

Comments are closed.