The House of Favourite Newspapers

Hackers Waondoa Wimbo wa Despacito YouTube!

Luis Fonsi

HATARI sana! Mtandao wa YouTube umeingiliwa na wadukuzi ‘hackers’ walioondoa wimbo uliofanya vizuri zaidi kwa kutazamwa na zaidi ya watu bilioni tano, Despacito.

 

Wimbo huo ulioimbwa na mwanamuziki Luis Fonsi, ulidukuliwa kwenye mtandao huo na wadukuzi hao kuweka picha ya watu waliovaa maski, huku wakiwa wameshika bunduki.

Baada ya kitendo hicho, mashabiki wengi waliandika kwenye mtandao wa Twitter wakitoa maoni yao na baadaye Mtandao wa YouTube, ulifanya juhudi na kuurudisha hewani.

 

Hata hivyo, iligundulika pia nyimbo za wanamuziki wengine kama Selena Gomez, Justin Bieber, Drake, Taylor Swift, Chris Brown, Shakira, DJ Snake na Katy Perry zilikuwa zimeondolewa, na YouTube waliweza kuzirudisha zote mtandaoni.

Comments are closed.