The House of Favourite Newspapers

HAKUNA MSANII WA KUFUNGIWA AKISOMA HII!

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe

TATIZO la wana-muziki na wasanii wengi Bongo hawapendi kujielimisha, hasa kwenye mambo yanayo-wahusu, jambo linalofanya wengi wajione wajuaji lakini wakizun-gumza au kulala-mikia jambo fulani unaona kabisa wapo nyuma ya ukweli.  Katika hili yapo mengi naweza kuyaeleza na mifano ya wasanii wengi, lakini sioni sababu ya kufanya hivyo zaidi ya kuwasilisha meseji kwa ujumla kwamba wasanii wanapaswa kujielimisha kwani itawasaidia kwenye kazi zao. Kwanza itawaepusha pia kwenye ugomvi na serikali, lakini ‘watamenteni’ mashabiki wao na kazi zao zitakwenda vizuri.

KWA MFANO, SUALA LA KUFUNGIWA VIDEO ZAO.

Ukweli ni kwamba kama wasanii wote wangekuwa na elimu hii hakuna ambaye angefu-ngiwa video yake na kupoteza muda, pesa kwa kazi ambayo haina manufaa! Nitakueleza zaidi. Jumanne wiki hii inayomalizikia ofisini kwetu kwenye Jengo la Global Group hapa Sinza Mori, tulikuwa na ugeni mkubwa wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.

Akiwa hapa, miongoni mwa mambo aliyoyazungumzia kwa kina ni kufungiwa kwa video za wasanii. Alieleza wazi pia kwamba katika kipindi cha miaka miwili wizara anayoisimamia kupitia watendaji wake wameweza kufungia video za wasanii 16 ambazo ni asilimia 0.13 ya nyimbo zote nchini, idadi ambayo ni ndogo na kwamba serikali imekuwa ikitoa elimu kabla ya kufikia hatua ya kufungia video. Kwa sababu alizoziweka wazi waziri Dk. Mwakyembe unaweza kusema ni ujinga wa wasanii au uvivu wao kujifunza ili kuwa ‘safe’ kwenye kazi zao.

IPO HIVI

Sheria za nchi zipo wazi kwenye sanaa kama alivyosema Dk. Mwakyembe. Ni kweli kwamba picha mnato (picha) au picha jongefu (video) zinazokiuka maadili haziruhusiwi. Kwa msanii anayefanya hivyo ni lazima atachukuliwa hatua na tumeona wanamuziki kadhaa wamekumbwa kwenye hili.

Tuna mifano ya Snura Mushi kwenye video yake ya Wimbo wa Chura na mwana-muziki Roma kwenye wimbo wake wa Kibamia na Daimond Platnums kwenye Wimbo wa African Beauty. Nyimbo zao zilifungiwa kwa sababu zilionekana hazina maadili. Lakini pamoja na kufungiwa, wasanii hao waliitwa na kuambiwa wabadilishe baadhi ya vitu ambavyo vilitoka nje ya mstari.

Snura na Roma, walizipiga chini video zao hizo na kusonga mbele na mambo mengine lakini Diamond alifanya ‘version’ nyingine ambapo ile ya kwanza aliita ‘Explicit 18+’ na nyingine ya pili aliita ‘clean version’. Hii ndiyo elimu ambayo wasanii wengi hawana na wangekuwa nayo basi kila kitu kingekuwa kinakwenda sawa.

EXPLICIT NI NINI?

Hili ni neno la Kingereza ambalo linatumika sana hasa kwenye mambo ya picha na video. Ukilifafanua maana yake ni ‘uwazi’, kwamba kitu kinac-hoonyeshwa bila kufichwa-fichwa. Kama kuna ‘scene’ za mapenzi, basi wataz-amaji huon-eshwa kila kitu kinavyo-endelea.

Kwenye sanaa maudhui haya yote yanaru-husiwa kuwa-silishwa. Lakini muwasilishaji hupewa masharti ya kulinda maadili kwa kuiachia video yake mitandaoni lakini pia mbele ya jina la wimbo ni lazima aandike neno ‘Explicit’ au ‘Explicit 18+’. Diamond alifanya hivyo kwenye wimbo wake wa African Beauty, na hakukuwa na tatizo lolote lile ingawa baadaye aliuondoa mitandaoni kwa mapenzi yake mwenyewe.

Ukitazama hata kwa upande wa wasanii wa ng’ambo ambao wasanii wetu wamekuwa wakiwapigia kelele kuwa mbona wao wanafanya video ‘chafu’ na hawafungiwi, si kweli. Asilimia kubwa huwa wanafanya video ‘version’ mbili, ‘explicit’ na ‘clean version. Clean version inakuwa ni kwa ajili ya media

na explicit kwa ajili ya mitandaoni kwa mashabiki ambao wanapenda kuona maudhui hayo ya kikubwa na kunakuwa hakuna tatizo na serikali wala hata Mtandao wa YouTube hauwezi kuifungia video ambao mbele imeandikwa explicit.

Na kusema kweli nyingi kati ya kazi hizo chafu zinazowekwa mitandaoni ndizo tunazonyonya huku kwetu na kudhani kwamba kwa jinsi zilivyo hata kwenye vyombo vya habari vya ng’ambo zinachezwa hivyo zilivyo jambo ambalo si kweli. Zipo video nyingi za wanamuziki Lil Wayne, Rick Ross, Criss Brown na wengine wengi za aina hii; hata kutoka hapa Afrika zipo mitandaoni na hakuna tatizo.

Hili ni suala ambalo hata waziri Dk. Mwakyembe alilizungumzia kwamba; mwanamuziki kama anahitaji kutoa video ya maudhui ambayo anaona hayatawapendeza watu wote afahamu namna ya kuyawasilisha, akiyapeleka huko mitandaoni kwa kufuata vigezo, serikali haiwezi kuinuka tu kufungia.

Kwa hiyo kina Roma wangefahamu juu ya hili na wengine, wasingekuwa wanapoteza pesa na muda kuandaa video zao hizo za explicit na wanataka zitumike kwenye vyombo vya habari, wangeandaa version mbili na mambo yangekwenda.

CLEAR VERSION

Hii ndiyo kama nilivyoielezea. Ni video safi ambayo mtu yeyote anaweza kuitazama.Kijana, mtu mzima na hata watoto. Kunakuwa hakuna ukakasi wowote pale mnapotazama mkiwa mmekaa pamoja.

Kwa hiyo, ni vizuri wasanii wakawa wanajielimisha zaidi kwenye mambo yanayowahusu itawasaidia sana. Mambo ya msanii kukurupuka na video za ‘kishamba’ halafu baadaye zikifungiwa; kelele zinakuwa nyingi hayakubaliki, kwa sababu serikali imeapa kulinda maadili ya watu wake.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.