The House of Social Media
gunners X

Halima Mdee: Sijaona Wakuniondoa Kawe – Video

0

Mbunge wa Kawe kupitia Chadema, ambaye pia ni Mwenyekiti wa BAWACHA Tifa, Halima Mdee amesema mpaka sasa bado hajaona mtu ambaye anaweza kumuondoa jimbo la Kawe.

 

Mdee amesema hayo leo Jumatano, Januari 8, 2020 wakti akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na kusema iwapo CHADEMA itashika dola mwaka 2020, watatua mzigo wa manyanyaso ya kiuchumi, kisiasa na kijamii wanayoyapata wanawake.

 

“Ulinzi wa mwanamke si kipaumbele tena kwa serikali ya CCM kwa sababu wanawake 150 wameuawa na waume zao kwa mwaka na hizo ni takwimu zilizoripotiwa.” 

 

“Kuna Dreamliner zimepaki pale Airport, nyingine hazijapata hata safari, na hata abiria hakuna, Watanzania ni wachache wenye uwezo wa kupanda Ndege, Mimi mwenyewe ni Mbunge kuna wakati napanda Ndege kishkaji yani, napanda kwa Manati.

 

“Tumeazimia kama BAWACHA, kuwa hatuwezi kuruhusu katika nchi yetu watu kumiminiwa risasi hadharani, watoto wetu wa kike kunyimwa fursa ya kupata elimu kisa tu wamebebeshwa mimba, Watanzania wanabambikiwa kesi za uhujumu uchumi kisa tu wanawakosoa watawala, hatuwezi.

“Tulishaona toka mwanzo ishara ya huyu kiongozi wa nchi aliyetangazwa na tume ya uchaguzi kuwa na viashiria vya udikteta, ndio maana tukatangaza ukuta, lakini wananchi hawakutuelewa. Watu wameondolewa kisa hawana vyeti feki bila uthibitisho, nadhani wananchi sasa hivi wameanza kuelewa kwanini tulitaka kufanya harakati ya ukuta.

 

“Hatuwezi kuruhusu kuwa na chaguzi za kihuni lakini Watanzania hawataki kuchukua hatua,wanaishia kuandamana Twitter na Facebook, kwenye nchi ambayo wananchi wamepigika lakini CCM inaongoza vijiji,vitongoji na mitaa kwa 100% kisa tu Rais ametoa maelekezo kwa watendaji.

 

“Ninajua Kabendera atatoka gerezani kwa sababu hana hatia, lakini tayari mama yake ameshafariki kwa sababu hakuweza kupata matunzo. Sugu alipowekwa gerezani mama yake alifariki kwa ‘Pressure’ baadae mahakama kuu ikasema hana hatia lakini tayari mama yake ameshafariki.

 

“Sekta za afya, kilimo na maji ndio zinagusa wanawake nchini, bajeti zake zimekuwa ni ndogo sana, kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa lakini kwenye bajeti kimetengewa bilioni 100 zikahudumie asilimia zaidi ya 80 ya Watanzania, lakini fedha zinazotolewa ni bilioni 2 tu.

 

“Kati ya watoto watano chini ya miaka 18, wawili wanaolewa wakiwa chini ya miaka 18. Haya ni mambo ambayo kama taifa tuyatafutie tiba, hali ni mbaya kiasi kwamba watoto hawaijui kesho yao,” amesema Mdee.

TAZAMA VIDEO AKIZUNGUMZA HAPA

Leave A Reply