The House of Favourite Newspapers

HARMONIZE, WOLPER KUKINUKISHA IDD PILI DAR LIVE (PICHA +VIDEO)

Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize (katikati) akiwa na Meneja wa burudani, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ (kulia).

 

Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize leo ametambulisha Usiku wa Kusi utakaofanyika siku ya Idd Pili katika Ukumbi wa Dar Live wakati akiongea na wanahabari katika ofisi ya Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar.

 

Msanii huyo amesema atafanya shoo ya aina yake siku hiyo na atasindikizwa na wasanii mbalimbali kutoka WCB.

Pia amesema kuwa, host wa shoo hiyo atakuwa msanii wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper, huku kiingilio cha shoo hiyo kikiwa 10,000/-

 

Mbali na shoo, Harmonize ameweka wazi mahusiano yake na baunsa wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Mwarabu Fighter kuwa hawana tofauti yoyote, maneno yaliyokuwa kwenye mitandao hayana ukweli wowote.

 

Pia amenogesha shoo hiyo kwa kusema kuwa, kampuni ya ulinzi ya Mwarabu Fighter ndo itafanya kazi siku ya shoo.

Comments are closed.