The House of Favourite Newspapers

HATIMAYE MAJIZZO AMTOLEA MAHARI LULU, NDOA YAO YANUKIA!

BAADA ya Staa wa Filamu BONGO, ‘Elizabeth Michael’ maarufu kama Lulu  kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Majizzo, usiku wa Septemba 30, mwaka huu, hatimaye wawili hao wamepiga hatua nyingine kuelekea kwenye ndoa yao.

Jana Jumapili, Novemba 18, 2018, Majizzo alimtolea mahari mrembo huyo ikiwa ni takribani siku tano tu baada ya kumaliza kifongo chake alichkokuwa akikitumikia kwa kosa la kumuua mwigizaji Steven Kanumba bila kukusudia.

 

Katika ukurasa wake wa Instagram, baada ya kumaliza kutoa mahari kwa familia ya Lulu, Majizzo ambaye pia ni mwanzilishi wa Radio EFM na TVE aliandika; “Deal Done” huku Lulu kupitia akaunti yake ya Instagram naye akiweka picha na Emoji yenye ishara ya mtu akifanya maombi na kumshukuru Mungu.

Mkuu wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda katika ukurasa wake wa instagram atoa pongezi kwa kuandika, “Mafanikio yenu yamebeba watu wengi, na kila hatua inaonyesha hamtanii basi Mungu wangu aendelee kuwaonyesha njia ili mfikapo mkawe msaada na kwawengine.”

 

Mastaa kibao walikuwepo kuhudhuria sherehe hiyo ya kutolewa mahali kwa Lulu jambo ambalo ni hatua mpya kuelekea ndoa yao inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Comments are closed.