The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Rais Jammeh ‘Amekubali Kuachia Madaraka’ Gambia

yahya-jammehGAMBIA: Hatimaye Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia, Yahya Jammeh (pichani) amekubali kung’atuka na kuondoka nchini humo, rais anayetambuliwa na jamii ya kimataifa amesema.

Rais aliyeapishwa juzi kwenye Ubalozi wa Gambia nchini Senegal, Adama Barrow ametangaza hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, baada ya mazungumzo ya saa kadha yaliyonuiwa kumshawishi Bw Jammeh kukubali matokeo ya uchaguzi. Mataifa ya Afrika Magharibi yamewatuma wanajeshi Gambia na kutishia kumuondoa Jammeh madarakani kwa nguvu.

barrowAdama Barrow alivyoapishwa kuwa rais wa Gambia.

Bw Barrow amekuwa nchini Senegal kwa takriban wiki moja.  ambako aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa Gambia mjini Dakar mnamo Alhamisi.

Bw Jammeh alikuwa amepewa muda wa kuondoka madarakani kufikia saa sita mchana la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambao taya wameshaingia nchini humo baada ya muda wake wa kuongoza kukamilika Jumatano ya juzi licha ya kufanikisha kulishawishi bunge lipitishe makubaliano ya yeye kuendelea kuwa madarakani hadi Mei.

Amekuwa akishauriana na Rais wa Guinea Alpha Conde na mwenzake wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz huku wanajeshi wa Ecowas kutoka Senegal na nchi nyingine za Afrika Magharibi waliingia nchini humo baada ya kuapishwa kwa Bw Barrow na walisema hawakukumbana na upinzani wowote.

Imeripotiwa kwa sasa hali huenda ikawa shwali baada ya rais huyo kukubali kung’atuka madarakani kwa amani ili amuachie mpinzani wake Adama Barrow ambaye amekwisha apishwa..

Comments are closed.