The House of Favourite Newspapers

HAWA APANGISHIWA HOTELI

Hawa Said

MSANII aliyepata jina kupitia Wimbo wa Nitarejea, Hawa Said baada ya kutua Bongo akitokea nchini India alipokwenda kwa matibabu, amepangishiwa hoteli ambapo atakaa kwa muda wa miezi mitatu ili kuepusha usumbufu.  Akizungumza na Risasi Jumamosi, mama wa Hawa, Ndagina Kapera alithibitisha mtoto wake kurejea salama kutoka nchini India alikokuwa kimatibabu akiwa na afya ambapo baada ya kutua amepangishiwa chumba hotelini kwa ajili ya kuepusha usumbufu wa kelele.

“Hawa amepewa masharti ya kukaa sehemu iliyotulia, isiyo na kelele kutokana na tatizo lake la moyo hivyo amepangishiwa hoteli moja hapa jijini Dar (jina linahifadhiwa) na meneja wa Wasafi (Hamis Taletale ‘Babu Tale’) kwa muda wa miezi mitatu mpaka afya yake itakapotengamaa,” alisema mama huyo.

Mama Hawa alisema anamshukuru Mungu mwanaye anaendelea vizuri, lakini watu anaowapa shukrani zake za dhati ni Babu Tale na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambao hana cha kuwalipa kwani wao ndiyo wamefanikisha matibabu ya mwanaye huyo.

STORI: Shamuma Awadhi, Dar

Comments are closed.