The House of Favourite Newspapers

HEMED ATAJA SIRI YA KUZAA NA WANAWAKE WA KAWAIDA

STAA wa filamu Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ ameeleza siri ya kuzaa na wanawake wa kawaida kwamba mastaa wengi wa kike hasa Bongo Muvi hakuona mwenye vigezo vya kuwa mama bora.

Akichezesha taya na Za Motomoto News, Hemed alisema kuwa kwa sasa ana watoto sita ambao amezaa na wanawake tofauti, lakini hakuwahi kuona mwanamke staa mwenye kigezo cha kuzaa naye kwani anapenda wanawake wanaojiheshimu na wenye mapenzi ya kweli.

 

“Ninamshukuru sana Mungu kwa kunijalia watoto sita kwa wanawake ambao hawana umaarufu hata mmoja maana wangekuwa mastaa tungesumbuana sana,” alisema Hemed.

Comments are closed.