SWETA LA HEMED LAZUA GUMZO

Hemed Suleiman

PENGINE hali ya hewa isiyotabirika jijini Dar es Salaam mara baridi mara joto ndiyo iliyomponza msanii Hemed Suleiman baada ya kuzuka msi­bani wakati wa jua kali akiwa na sweta na kuzua gumzo.

Za Motomoto News lilikuwa shuhuda wa tukio hilo kwenye msiba wa mtoto wa Muna uliofan­yika wikiendi iliyopita Dar, kwa kuwaona baadhi waombolezaji wakikodoa macho na kuachia wazi midomo yao huku kiulizo kikiwa: “Kulikoni huyu msanii na sweta kwenye jua kali na joto jingi?”

“Ubishoo tu huu.”

“Jamani tusihukumu yawezeka­na ana sababu za msingi za kuja na sweta.” Vi­onjo vya mijadala kutoka kwa baa­dhi waombolezaji waliofurika kumuaga mtoto huyo eneo la Viwan­ja vya Leaders Club vilisikika.

Hata hivyo baada ya shu­ghuli ya kuaga kumalizika safu hii ilimsaka Hemed lakini haikufanikiwa; lengo ni kumhoji ku­likoni sweta wakati wa jua kali, tena msibani?

 Stori : NA HAMIDA HASSAN

Toa comment