The House of Favourite Newspapers

Hii Ndo Sababu Ya Wasichana Wengi Kutokuolewa

Kila jambo linalotokea kwenye maisha lazima litakuwa na sababu, nikimaanisha pia hata mschana mzuri mwenye vigezo vyote akishindwa kuolewa pia kuna sababu.Waschana wengi wa siku hizi wamekuwa wakilalamikia swala katika mahusiano kwamba hayadumu na huishia kuachwa.

Wewe ni mschana mzuri na kuolewa ni haki yako, endapo utazingatia mambo yaliyoandikwa hapa na kujirekebisha basi mchumba utakayempata wakati huu ni lazima atakuwa mume wako.

1. VIGEZO VISIVYO NA MSINGI.

  • Kuweka vigezo vingi na kuchagua chagua sana inaweza ikawa ni sababu ya kufanya mabinti wengi wasiolewe.
  • Binti unakuta anataka mwanaume awe amesoma, mrefu, handsome, sijui awe na kazi nzur, awe na upendo wa kweli, na mambo mengi kama hayo.

Wanaume wanaokidhi vigezo hivyo ni wachache sana na kimsingi inawezekana wasiwepo kabisa. Mwisho hujikuta umri unaenda bila ya kuolewa au kuangukia kwenye mikono ya Wanaume ambao ni matapeli wa mapenzi.

Kuna msemo usemao, “ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu” na mwingine ufananao na huo unaosema “mchagua nazi hupata koroma”.

2. NAMNA UNAVYOJIWEKA.

  • Jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia. Mavazi unayovaa, marafiki ulionao na hata tabia yako kwa ujumla.
  • Mabinti wengi wanafeli sana kwenye eneo la mavazi, mavazi ya kuacha maungio ya ndani wazi yanawashushia heshima mabinti wengi sana bila wao kujua, wengi wanaona kama wanaenda na wakati lakini wanajidhalilisha.
  • Hakuna mwanaume anayependa kuoa mwanamke asiyejiheshimu, kama yupo basi hatakuwa muaoji. Mwanaume gani anayependa kutembea na mkewe akiwa maziwa yapo wazi yananing’inia kama yanataka kuanguka? Sketi fupi mapaja yote yapo wazi na tena ina mpasua? Suruali imembana mpaka maumbile ya ndani, michirizi ya nguo ya ndani inaonekana.
  • Hakuna mwanaume anayependa mwanamke ambaye mwili wake ni maonyesho ya saba saba labda kama sio muoaji
  • Hakuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye hata nyumbani kwao hana ujasiri wa kumpeleka labda kama sio muoaji
  • Hakuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye starehe yake ya usiku na Mali yake ipo wazi kwa marafiki zake na watu kama Mali ya umma labda kama sio muoaji.

MUHIMU: Dada zangu,ukivaa mavazi ya ajabu ajabu utavutia Wanaume wa kulala na wewe na kukuacha na si waoaji, utakuwa ni kiburudisho cha usiku mmoja na si mwanamke wa maisha.

3. MANENO UNAYOJITAMKIA.

  • Vijana wengi wamekuwa na desturi ya kujisemea maneno ya laana bila kujua yana madhara gani katika maisha yao kama (Wanaume wote ni wale wale, sijui siku hizi Hakuna waoji, mara Wanaume wote ni waongo, baba mmoja na mama mmoja.Kinywa chako kina uwezo wa kuumba. Kila neno baya au zuri unalojitamkia ndivyo litakuwa kwako.
  • Kama Unasema Wanaume wote ni waongo basi usishangae Kila mwanaume atakayekuja kwako akiwa muongo. Kama Unasema sina shida ya kuolewa basi miaka 30 itakukuta ukiwa nyumbani kwa baba yako. Chunga kinywa Chako.

4. KUTOKUSHUKA.

  • Utii ni tatizo kwa mabinti wengi sana wa sasa. Wengi hawakubali kushuka, hawataki Kuongozwa wanataka kujiongoza wenyewe.
  • Kumtii mwanaume wanaona kama ni jambo la kizamani, wanaita mfumo dume hivyo wanataka kuishi katika mfumo Jike.
  • Hakuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye si msikivu (jike dume), kama hautaki Kuongozwa basi wewe ni mwanaume sasa unataka mwanaume wa nini?

5. MAAGANO ULIYOWEKA HUKO NYUMA.

  • Kama kuna mtu mliahidiana kuwa mtaona halafu kwa sababu zisizo na msingi ukamuacha, basi hii inaweza ikawa ni moja ya sababu ya kukufungia baraka yako ya ndoa.
  • Kama kuna mtu ana nung’unika kwa ajili yako, kama kuna mtu ana lia kwa ajili yako huu unaweza ukawa mwiba kwako usiifikie ndoa au ukaifikia lakini isiwe salama.
  • Kama kuna watu ulishindwa kutimiza ahadi uliyowaahidi unatakiwa kutubu dhambi hiyo na kutengeneza nao kwa kuwaomba msamaha ili usiwe na vifungo vinavyokuzuia.

6. KUKOSA MSIMAMO.

Mabinti wengi sasa hawana msimamo linapokuja swala la kujizuia kufanya mapenzi.Asilimia kubwa ya waschana wanalalamika kuumizwa na wapenzi wao huku kwa upande wa pili wakiwa tayari wameshakutana kimwili.

Kama mwanaume umeshampa mwili wako ni nini tena atakachokihitaji kutoka kwako? Kama ameshakula sebuleni kuna haja gani ya kuingia Jikoni?

Kuna asilimia ndogo sana ya wanaovua sketi zao na mwisho wa siku wanavaa gauni (Shela) la ndoa, hakikisha tu unakuwa makini na mwanaume wako.

Endpo utazingatia mambo 6 muhimu hapo juu na kuchukua tahadhari, hautopata shida katika mahusiano yako, kwasababu maisha mazuri ya ndoa ndyo maisha yatakayokusaidia ndoa yako kuwa na furaha na amani.

EXCLUSIVE: ANNA JUAKALI AMKABIDHI MUNGU NDOA YAKE, AFICHUA ya UHUSIANO -”NAISHI MAISHA MATAKATIFU”

Comments are closed.