The House of Favourite Newspapers

Hispania na Brazil Zatangaza Kesi ya Kwanza ya Kifo cha Homa ya Nyani

0
Ugonjwa huu ulianzia nchini Uningereza mnamo mwezi Mei mwaka huu

NCHI za Hispania na Brazil zimetangaza kesi za kwanza za vifo vya homa ya nyani tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea mapema mwezi Mei.

 

Kwa Mujibu wa Wizara ya Afya ya nchi ya Hispania katika kitengo cha magonjwa ya dharula imeripoti jumla ya kesi 4,298 ambapo jumla ya kesi 120 sawa na 3.2% wagonjwa wameripotiwa kulazwa.

Kesi za virusi vya homa ya nyani zimeshamiri zaidi katika miji ya Sao Paulo na Rio de Janeiro

Mtu aliyeripotiwa kufariki nchini Brazil ni mwenye umri wa miaka 41 ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali kwenye mji wa Belo Horizonte nchini humo, ingawa taarifa zinadai kuwa mgonjwa huyo alikuwa na matatizo mengine ya upungufu wa seli za kinga ya mwili.

 

“Ni muhimu kutambua kuwa mgonjwa huyu alikuwa na tatizo jingine la upungufu wa seli za kinga mwilini ili kutosababisha taharuki kwa jamii, kiwango cha vifo ni kidogo sana.” amesema Katibu wa Wizara ya Afya Fabio Baccheretti.

Tayari WHO imetangaza ugonjwa huu kama Janga la Kidunia

Wizara ya Afya ya nchini Brazil imebainisha kuwa imerekodi zaidi ya kesi 1,000 za virusi vya homa ya nyani ambapo kesi nyingi zimepatikana Jiji la Sao Paulo pamoja na Rio de Janeiro.

Leave A Reply