The House of Favourite Newspapers

Historia ya Maisha ya ALIKIBA Tangu Kuzaliwa – Video

STAA wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ alizaliwa na wazazi wake Bi. Tombwe Njere na Mzee Saleh Omari, mkoani Iringa mnamo Novemba 26, 1986. Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne kwenye familia yao, akifuatiwa na Abdu Saleh Kiba ambaye pia ni mwanamuziki, Zabib Kiba (dada yake) na Abuu Kiba (mdogo wao wa kiume wa mwisho).

 

Muziki ni kati ya vitu ambavyo zimekuwa vikipendwa na mwanamuziki huyu tangu utoto wake. Asilimia kubwa ya wapenda burudani Afrika Mashariki kwa sasa wanazungumzia kuhusu ujio wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Alikiba.

 

Baadhi ya watu wamekuwa wakimlinganisha na mwanamuziki nyota kwa sasa Diamond Platnumz, ambaye naye kwa sasa yupo katika nafasi ya juu kimataifa kama ilivyo kwa Alikiba.

 

Si kwamba ndiyo anaingia katika muziki, kwa watu wanaojua historia ya bongo fleva wanakumbuka kwamba kijana alikuwa tishio, kwani amekuwapo kwenye gemu tangu mwaka 2004 na kufanikiwa kutoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimtambulisha uliojulikana kama ‘Cinderella’ alioutoa mwaka 2006.

 

Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita mwaka 2004, alianza kujituma katika muziki na kufanikiwa kuandika wimbo wake wa kwanza, ‘Maria’. Mwaka huohuo Alikiba alianza kutengeneza albamu yake ya kwanza. Ilipofika mwaka 2005, alipata ofa ya kwenda kuchezea soka la kulipwa nchini Uganda, lakini baadaye aliachana na mpira ili kuendeleza kipaji chake cha muziki.

 

Mwaka 2006 alifanikiwa kuachia albamu iliyopewa jina la ‘Cinderela’, sambamba na kuachia wimbo huo redioni, ambao ulivuma na kusababisha albamu hiyo kuuzika zaidi sokoni. Albamu hiyo ilikuwa ni kati ya albamu bora na iliyouza zaidi mwaka 2006 Afrika Mashariki.

 

Tangu hapo akaanza kupokea mialiko mingi kutoka Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi. Aliifanya Afrika Mashariki kumjua kwa muda mfupi kupitia vibao kadhaa vilivyokuwepo katika albamu hiyo kama MacMuga, Nakshi Mrembo, Njiwa na Mali Yangu.

 

FUATILIA SIMULIZI YA MAISHA YA ALIKIBA HAPA

Comments are closed.