HUSNA MAULID: UYATIMA UMENIFUNDISHA MAISHA

MREMBOambaye amewahi kushiriki mashindano mbalimbali ya urembo nchini Husna Maulid, amesema uyatima umemfanya ayajue maisha mapema kwani mpaka sasa angekuwa hajaanza kujitegemea.

 

Akizungumza na SHUSHA PUMZI, Husna alisema kuwa kabla mama yake hajafariki alikuwa akimfanyia kila kitu, lakini alipotangulia mbele za haki, ndipo akili ilipotambua yuko peke yake na anahitaji kufanya awezalo ili maisha yaende.

 

“Baada ya kuwapoteza mama na baba nilikua mkubwa ghafla, kwa maana nilianza kukimbizana na majukumu yaliyokuwa makubwa kuliko umri wangu na mpaka sasa nimekomaa kabisa na ninayajua maisha ipasavyo,” alisema Husna.

Toa comment