The House of Favourite Newspapers

Huyu Ndiye Mwanamme Mwenye Nywele Nyingi Zaidi Duniani

Yu Zhenhuan.

Mtandao wa World Ranking umemtaja Yu Zhenhuan wa China kuwa ndiye mwanaume mwenye nywele nyingi zaidi duniani.

Mwili wa Yu Zhenhuan umefunikwa na nywele nyingi tofauti na binadamu wengine hali iliyosababishwa na yeye kuwa na ugonjwa unaofahamika kama Hypertrichosis.

Unaambiwa kwa sasa anataka kuondoa sehemu muhimu ya nywele kutoka kwenye mwili wake lakini nywele zote zitahitajika kuteketezwa kwa laser na utaratibu huu utamsababishia maumivu makali sana katika mwili wake.

Yu Zhenhuan akiwa na mpenzi wake.

Yu Zhenhuan amekuwa kwa muda mrefu anaishi na mkewe ambaye amekuwa akimsaidia kupata njia ya kumwezesha kupunguza nywele katika mwili wake huo.

Comments are closed.