The House of Favourite Newspapers

Huzuni…Familia ya Hoyce yanusa kifo ajalini

1

HOYCE TEMU (1) Mama mzazi wa Hoyce Temu

IMELDA MTEMA, Amani

Dar es Salaam: Familia ya Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwemo mama yake mzazi, dada zake watatu na mdogo wake, wamenusurika kupoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria, kupata ajali mbaya kwenye makutano ya Barabara za Ali Hassan Mwinyi na ile ielekeayo kwenye Ufukwe wa Coco, Amani linakujuza.

HOYCE TEMU (2)Ajali ilivyotokea

Akizungumza kwa masikitiko, Hoyce alisema ajali hiyo ilitokea mchana wa Jumapili iliyopita wakati wanafamilia hao wakielekea Ufukwe wa Coco kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ambapo ghafla, gari jingine aina ya Range Rover Vogue, lililigonga gari walilokuwemo ndugu zake na kuwasababishia madhara makubwa.

Hoyce aliongeza kuwa alipata taarifa za kupata ajali ndugu zake hao wakati akiwa Bagamoyo, Pwani kwenye kambi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi.

hoyce temuMiss Tanzania 1999, Hoyce Temu

Mrembo huyo alisema kuwa alipigiwa simu na dada yake mkubwa aitwaye Edith aliyekuwa kwenye ajali hiyo na kumtaarifu kwamba wamepata ajali mbaya na hali ya mama yao siyo nzuri, jambo lililomlazimu kurejea haraka jijini Dar es Salaam hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili walikokuwa wamelazwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilitokea baada ya kijana mwenye asili ya Kisomali, aliyekuwa akiendesha Vogue, kuvunja sheria za barabarani kwa kuendesha kwa mwendo kasi na kusababisha aligonge gari hilo, lililokuwa likiendeshwa na mdogo wa Hoyce aitwaye Rachel.

Baada ya kufikishwa Muhimbili, majeruhi wote walipatiwa matibabu ya awali na kulazwa kwenye Wodi ya Kibasila ambapo wawili waliruhusiwa kutoka na wengine wawili, akiwemo mama yake mzazi, walibaki hospitali.

“Kwa kweli ilikuwa ni ajali mbaya sana, namshukuru Mungu kwani ningepoteza familia yangu yote na hapa bado namuuguza mama yangu na ndugu zangu ingawa wengine wanae-ndelea vizuri,” alisema Hoyce.

1 Comment
  1. annie says

    POLENI SANA, MUNGU ATAWAAFU. HUYO ALIYEWAGONGA KAMA NI UZEMBE ACHUKULIWE SHERIA

Leave A Reply