The House of Favourite Newspapers

Ikulu Yafafanua Siku 4 za Maombolezo

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa amefafanua juu ya siku 4, za maombolezo ya ajali ya MV-Nyerere zilizotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli na kusema kuwa shughuli za kila siku zitaendelea kama kawaida.

 

Ufafanuzi huo umekuja kufuatia kuzuka kwa sintofahamu juu ya uwepo wa mapumziko ya kazi siku ya Jumatatu ya tarehe 24 kufuatia tangazo la Rais alilolitoa jana juu ya kuwepo kwa maombolezo ya ajali ya Mv-Nyerere iliyotokea juzi.

 

Gerson Msigwa ameandika “Napenda kutoa ufafanuzi kuwa Jumatatu tarehe 24 Septemba, 2018 ambayo ni siku ya mwisho ya maombolezo ya Kitaifa, itakuwa ni siku ya kazi kama kawaida.”
“Mhe. Rais Magufuli ametangaza siku 4 za maombolezo na sio za mapumziko” ameandika Gerson Msigwa.

 

Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alagiza viongozi wa taasisi na mamlaka zinazosimamia usafiri wa majini wahojiwe na watakaobainika kuhusika kwa uzembe wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Comments are closed.