The House of Favourite Newspapers

India Imegoma Kutuma Madaktari Wake Kenya

kenya-na-india
New Delhi:
SERIKALI ya India imelikataa ombi la Serikali ya Rais Uhurua Kenyatta wa Kenya la kutuma madaktari wake ili wakatoe huduma ya afya nchini humo kufuatia mgomo wa madaktari wa Kenya zaidi ya 4,500 unaoendelea kwa zaidi mwezi mmoja sasa.

Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi jana kuwa serikali yake haiwezi kupeleka madaktari wake kwenye nchi hiyo ya Mashari mwa Afrika ambayo tayari inaonekana kuna matatizo kwenye sekta ya afya kwa zaidi ya miongo kadhaa sasa.

Wakati huo, madaktari sita wa Chama cha Madaktari Kenya wamesimamishwa kazi kwa mwezi mmoja kwa kukataa kusitisha mgomo huo ambao bado unaoendelea.
CREDIT: THE TELEGRAPH

Comments are closed.