The House of Favourite Newspapers

Jembe Jipya Yanga SC Kuanza Kazi Na Wanajeshi

Mwinyi Zahera

KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongoman, Mwinyi Zahera amemjumuisha kiungo wake mkabaji, Mohamed Issa ‘Banka’ kwenye orodha ya wachezaji waliongia kambini katika kujiandaa na michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

 

Yanga imeingia kambini juzi Juma­tano kwenye Hoteli ya Nefaland iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mazoezi ya mwishoni kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, Dar kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la FA uliotarajiwa kupigwa jana dhidi ya Biashara United.

 

Banka ambaye anasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Yanga akiwa uwanjani, ni baada ya kifungo chake cha mwaka mmoja kuelekea ukingoni alichokuwa anakitumikia kutoka Fifa baada ya kubainika alikuwa akitumia kilevi chenye asilimia 150.

 

Akizungumza na Championi Iju­maa, mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema kiungo huyo adhabu yake inatarajiwa kumalizika Februari 8, mwaka huu, hivyo ataanza kucheza katika mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tan­zania inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) utakaopigwa Februari 10, mwaka huu.

 

Saleh alisema kiungo huyo ni kati ya wachezaji waliongia kambini katika kujiandaa na mchezo wa Kombe la FA waliotarajia kucheza nao jana, licha ya yeye kutokuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mechi hiyo kutokana na adhabu yake kumalizika wiki ijayo.

 

Aliongeza kuwa, kiungo huyo tayari ameingizwa kwenye mipango ya Zahera katika michezo ijayo ya ligi ukiwemo wa Simba na Yanga utakao­pigwa Februari 16, mwaka huu kuto­kana na mazoezi anayompa.

 

“Baada ya mechi ya Biashara tutasa­firi naye kesho (leo) kuelekea Tanga kwa ajili ya mchezo ujao wa ligi dhidi ya Coastal Union na baadaye tutak­wenda naye tena Singida kucheza na Singida United, Februari 6.

 

“Mchezo huo wa Singida ndiyo utakuwa wa mwisho kutumikia adhabu na baada ya hapo atakuwa huru na kuanza kucheza katika mechi inayofuatia ya ligi dhidi ya JKT Tan­zania kabla ya kukutana na Simba,” alisema Saleh.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.