The House of Favourite Newspapers

JERRY  MURO: ARUMERU YA WAKULIMA, WAFUGAJI INAKUJA

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jery Muro akizugumza jambo.
Akiwa na baadhi ya wakulima.

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jery Muro amejitolea  kuwasadia kuandika maandiko ya kibiashara wananchi wanaotaka kufanya Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara ili waweze ‘KUKOPESHEKA’ na taasisi za kifedha ambazo kabla ya kutoa msaada au mkopo huitaji mchanganuo au andiko la kibiashara kwanza kabla ya kuwawezesha wananchi ambao wanataka kuanza kilimo au ufugaji wa kibiashara.

 

 

 

Muro amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa ‘VIKWAZO’ vya maandiko ya mradi katika hatua za awali pindi wananchi wenye nia ya kuanzisha kilimo na ufugaji wa kibiashara wanapoanza safari ya kutimiza ndoto zao za kuwekeza katika sekta hizo, ambapo baada ya kubaini uwepo wa ‘vikwazo’ hivyo aliamua kujiongeza Kwa kutafuta wadau ambao atashirikiana nao katika kuwasaidia wananchi kuondoa vikwazo hivyo.

 

 

 

Jerry Muro amesema tayari kampuni binafsi ya wawezeshaji wa wakulima ( PASS) Private Agricultural Sector Support imekubal kuwaandalia na kugharamikia mpango kazi wa kibiashara (Bussiness Planning) zitakazowasaidia wakulima na wafugaji katika kupata mkopo katika Taasisi za Kifedha hali ambayo itawasaidia katika uendelezaji wa kilimo chenye tija na ufugaji wa kibiashara.

 

 

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Mhe Muro kufunga maoyesho ya jukwaa la wakulima Meru ambayo yamefanyika kwa siku tatu na kuwaleta pamoja wakulima, wafugaji na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo pamoja na kukubali kutoa msaada wa bure katika kuandaa na kuandika maandiko ya mchanganuo wa kibiashara pia amewapatia chumba Cha ofisi ya kuratibu na kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa haraka zaidi, na kuahidi kuwatafutia kompyuta kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za taarifa za wakulima na wafugaji.

 

Kwa upande wake Meneja wa Tawi la kampuni ya (PASS) amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumerry, Jerry Muro Kwa kuonyesha kuwajali wakulima na wafugaji ambapo amewataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi ili waweze kunufaika kupitia na Taasisi hiyo.

 

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

 

Comments are closed.