The House of Favourite Newspapers

JKT Queens Wana Jeuri Hao!

Kikosi cha timu ya JKT Queens.

WAKATI leo wakishuka uwanjani kuwavaa Mapinduzi Queens, uongozi wa JKT Queens umesema mazoezi ya kijeshi wanayofanya ndiyo kitu wanachojivunia kwa kuwa wanakuwa na uwezo wa kupambana kwa zaidi ya dakika 90 wawapo uwanjani.

 

Mabingwa hao watetezi wa ligi hiyo ya Wanawake, wameanza kwa kasi zaidi msimu huu na tayari wameshagawa dozi ya mabao 15 kwenye mechi mbili wakiwa na alama zao sita kileleni na kuwapiga bao wapinzani wao wa karibu ambao ni Yanga Princess, na Simba Queens

Simba Queens leo watakuwa Uwanja wa Karume kuvaana na Alliance Girls ya Mwanza, huku michezo mingine ni Panama Fc dhidi ya Baobab Queens, Marsh Queens na Evergreen,Mlandizi Queens dhidi ya Sisterz FC na Yanga Princes watavaana na Tanzanite SC hapo kesho Uwanja wa Karume.

 

Msemaji wa JKT, Elizabeth Buliba alisema, wao ni wanajeshi kwa hiyo lazima wapambane ili kuonyesha utofauti kwa timu zingine ambazo hazimilikiwi na jeshi huku akiweka wazi kuwa hakuna timu yoyote ambayo itaweza kupata pointi pindi watakapokutana.

Comments are closed.