The House of Favourite Newspapers

JKT Queens ‘Yaitafuna’ Simba Queens 1-0

JKT Queens wakishangilia baada ya kutupia bao dhidi ya Simba Queens.

KIKOSI cha Simba Queen jana kimepoteza mchezo wake wa kwanza mbele ya JKT Queens katika mchezo wa Ligi ya Wanawake maarufu kama Serengeti Women’s Premier League uliochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Mchezaji wa JKT Queens akiwatoka wachezaji wa Simba Queen.

JKT Queens waliandika bao dakika ya 45 baada ya mabeki wa Simba Queens kufanya uzembe na kumpa nafasi Anastazia Omary kuandika bao ambalo lilidumu kwa dakika 90.

 

Kocha wa Simba Queens, Mussa Mgosi,  amesema bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa ligi inaendelea

Kocha wa JKT Queens, Ally Ally, amesema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa ila wamefanikiwa kupata matokeo mazuri.

“Simba ni timu bora,  imepambana ila tumepata matokeo tumeweza kushinda, tunahitaji kutetea ubingwa wetu tena msimu huu,” alisema Ally.

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

 

Comments are closed.