Airport Wajibu Tuhuma za Ray Kuhusu Udokozi Uwanjani Hapo

Uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere umewataka abiria wanaodhani wamepoteza vitu vyao wakati wanasafiri kwa kutumia Uwanja huo watoe taarifa mapema ili waweze kusaidiwa kupata vitu vilivyopotea.

 

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Paul Rwegasha amesema iwapo mtu atapata tatizo lolote ni vyema akawasiliana na uongozi badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii kwani atakuwa anaichafua nchi.

Rwegasha amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya uwepo wa taarifa za Msanii Maarufu wa Filamu nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’ kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram akieleza aliibiwa vifaa vyake akiwa anaelekea Dubai.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment