The House of Favourite Newspapers

JOKATE AMUELEZEA MISS TZ BALAA LA MITANDAO

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’,

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita baada ya kumalizika kwa Shindano la Miss Tanzania 2018, alimueleza mshindi wa kinyang’anyiro hicho, Queen Elizabeth kutoka Dar balaa la mitandao ya kijamii na namna inavyoweza kumbomoa au kumjenga. Akipiga stori na Za Motomoto News, Jokate alisema baada ya kushinda, Queen Elizabeth amekuwa staa mpya kwa hiyo ategemee kusikia mengi kutoka mitandaoni ikiwemo

“Kikubwa unatakiwa kuwa tayari kupokea kila kitakachokuja kwako. Kwa sababu wakati mwingine unaweza kutukanwa kiasi kwamba ukatamani uachane na mitandao hiyo. “Lakini unatakiwa kufahamu hiyo ni hali ambayo inawakuta wengi wetu. Kwa hiyo kuwa mvumilivu na kwa upande wako itumie mitandao kwa manufaa ya jina na kazi zako,” alisema Jokate.

Stori: Boniphace Ngumije, Dar

Comments are closed.