The House of Favourite Newspapers

Jordin Sparks Amweka Hadharani Mtoto Wake

MWANAMUZIKI wa Marekani, Jordin Sparks,  na mumewe, Dana Isaiah, ‘wamemfichua’ kwa mara ya kwanza kwenye mitandao mtoto wao wa kiume aliyezaliwa Mei 2 mwaka huu.

Katika posti moja, Jordin alimwonyeshamtoto huyo aitwaye Dana Isaiah Thomas Jr., akiwa anatabasamu huku amevaa fulana ya kutokea shingoni hadi magotini (bodysuit) iliyoandikwa “mommy loves me” .

Aliandika chini ya picha hiyo: “Tabasamu hili daima liko moyoni mwangu. Mimi ni tone la maji kwenye sakafu.  Siwezi kuamini nimepata baraka na heshima ya kuwa Mama. Wow…Mungu ni mwema sana! 🦋😭

 

Comments are closed.