The House of Favourite Newspapers

JPM Awamaliza Sanchoka, Sasha!

Rais John Pombe Magufuli.

DODOMA: Rais John Pombe Magufuli ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na mamlaka zingine zinazohusika, kuwachukulia hatua kali wasanii wanaopiga picha nusu utupu na kuzitupia katika mitandao, sambamba na wale wanaocheza hivyo katika video, ambao miongoni mwao, wapo Sanchoka maarufu kama Sanchi, Sasha na Amber Lulu.

 

Akizungumza jana wakati akihutubia mkutano wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi (CCM) mjini Dodoma kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa jumuiya hiyo, alisema ni aibu kwa wazazi kuangalia vitendo hivyo vikifanyika bila hatua kuchukuliwa.

 

Sanchoka.

“Baadhi ya maadili yameanza kupotea, na nyie kama wazazi mmeshindwa kuyakemea haya. Kila unapofungulia mziki ukitaka kuwaona wanaocheza utakuta wanawake tu ndiyo wako uchi, lakini wanaume hapana, baadhi ya wanawake wanaachia viungo vyao.

 

“Kwa nini uwavulie hata wasiohitaji kuona uchi, tena kwa wakati ambao siyo muafaka? Nyinyi kama Jumuiya ya Wazazi imefika wakati mnapaswa kuyakemea haya. Tunaelekea wapi sasa? Tunawafundisha nini watoto wetu? Kwani akicheza amevaa nguo hatafurahisha?

Sasha

“Hata Adamu alipofanya dhambi alijiona yuko uchi, lakini hawa hawajioni wako uchi hata kama wanacheza miziki hadharani. Ifike wakati sisi kama Watanzania tuyalinde maadili yetu. Vya kukopi na kupesti tuviache. Yanayofanyika ni aibu.

“Vyombo vyetu vya habari, wasimamizi wa maadili haya wako wapi? Wizara inayosimamia haya wako wapi? Je, TCRA yenye mamlaka ya kufungia hata Televisheni inayorusha video za utupu wako wapi?” alihoji Rais Magufuli.

 

Baadhi ya wasanii ambao wanasifika kwa kutupia picha za aibu katika mitandao ya kijamii licha ya watatu hao ni pamoja na Faiza Ally, Gigy Money, Pretty Kind, Kidoa na wengine wengi.

Comments are closed.