The House of Favourite Newspapers

JUMA NATURE KUONYESHA UKONGWE WAKE KESHO

Related image
Juma Kassim ‘Juma Nature

NGULI kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Juma Kassim ‘Juma Nature’, kesho anatarajia kuangusha shoo ya kibabe kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live katika Tamasha la Kuwashukuru Watanzania lijulikanalo kama Tusua Maisha na Global ambapo ameahidi kuonyesha ukongwe wake kwa kuwafunika Man Fongo na Roma Mkatoliki.

Akipiga stori na ukurasa huu wa burudani, Juma Nature alisema kwamba mashabiki wake wanajua siku zote anachofanya anapokuwa na maiki mkononi na kesho ni nafasi nzuri kushuhudia makamuzi ya nguvu atakayoyafanya.

“Kesho Dar Live, nitaonyesha ukongwe wangu. Mashabiki wangu waje kwa wingi kwa sababu kwanza shoo ni bure na ninawahakikishie wataona tofauti ya mkongwe na wasanii wengine,” alisema Sir Juma Nature.

Comments are closed.