The House of Favourite Newspapers

Mzungu Aliyenusurika Kupikwa Supu Asimulia Mazito, Kabila la Wala Watu-7

TUNAENDELEA kuwasimulia habari ya kweli kuhusu makabila ya jamii moja katika nchi ya Papua New Guinea inavyokula watu; endelea. Kabla ya kuanza kuelezea jinsi watoto wao wadogo wa kiume wanavyowafanya nisimulie kwanza Mzungu mmoja mtalii, Muingereza Matthew Ilone akiwa na mchumba wake Clemens walivyookoka kuliwa na watu hao mwaka 2012, ni miaka mitano tu iliyopita, anasema:

“ Tulikwenda katika nchi hiyo na siku moja tulikwenda katika vijiji hivyo nikiwa na mchumba wangu. Watu hao walikuwa  wanatisha sana kwa jinsi walivyovaa mavazi yao ya asili, walituzunguka wakatengeneza mduara. Matthew aliliambia Gazeti la Sun.

“Walinifuata mimi wakararua fulana yangu kisha wakanifunga usoni, nikawa sioni! Nikawa na wazo kwamba inawezekana siku hiyo walituweka katika orodha ya vyakula vyao (Menu).

“Kifupi tuliogopa sana, kwa kweli tulikuwa katika mikono yao na tulikuwa tukiomba watuonee huruma wasitufanye kitoweo. Nilijua huo ndiyo utakuwa mwisho wetu katika msitu huo na hatutaonekana tena,” alisema Matthew. Matthew anasema aliwahi

kusikia simulizi juu ya wala watu hao na siku hiyo alijua kwamba wataliwa kwani mwaka huo wa 2012 waliwahi kupata habari ya binadamu kuliwa na watu hao. Hata hivyo, alisema watalii wengi huwa hawaamini kwamba katika miaka hii ya maendeleo kuna watu wanaweza kukamata binadamu wenzao na kuwaua kisha kuwala nyama kwa kuchemsha viungo vyao kama supu ya ng’ombe au mbuzi. Matthew na mchumba wake Clemens, walikutana kwa mara ya kwanza nchini Marekani, Los Angeles wakaamua kwenda katika visiwa hivyo kwa lengo la kujifunza baada ya kupata habari hizo.

Matthew Ilone muingereza aliyenusurika kupikwa supu

Waliambiwa kwamba watu hao huwa wanaua wenzao na kuwala ubongo kwa kuuchemsha.

“Tuliambiwa ubongo wa binadamu wakishaua mtu huushindilia kwenye mianzi na kupikwa na baada ya kuiva mianzi hupasuliwa na kuula kama watu wanavyokula soseji,” alisema.

Alisema kazi ya kuweka ubongo kwenye mianzi mara nyingi hufanywa na wanawake wazee ambao hupelekwa kwenye nyumba iliyolazwa maiti na kisha kichwa ‘kubanguliwa’ na kutolewa ubongo.

Kabila la wala watu

Kwenye sherehe za watoto kutoka jandoni, wanawake hao wazee huwa wanakwenda na ubongo huo wa binadamu na kuwagawia watoto ambao hufurahia bila shaka wakiwa hawajui kwamba wanachokula ni viungo vya binadamu wenzao.

Waliambiwa kwamba baadaye wanaume huchukua mwili na kukatakata tayari kwa kupikwa na kitu pekee ambacho hawali katika mwili wa binadamu ni kibofu cha mkojo. Watu hao wa Kabila la Kiru wanaamini kwamba kwa kula ubongo wa Mzungu, mizimu yao inafurahi na kuwalinda zaidi na huwa ni kinga wasipatwe na majanga.

Watoto wa kiume wanapopelekwa jandoni, hupakwa rangi nyeusi usoni na hutahiriwa kikatili na ngariba wao  baada ya kutahiriwa hunyolewa kichwani kama mtu mwenye kipara kwa kumaanisha kuwa sasa wamekuwa wazee na nywele zao zilizonyolewa kichwani kwa kutumia kisu kikali kugandishwa kwenye kidevu, hivyo kuonekana kama wana ndevu.

Baadaye hupewa zawadi yao kubwa baada ya kukaa jandoni na kupona ambayo ni huo ubongo wa binadamu unaoandaliwa na bibi vizee. Itaendelea wiki ijayo.

 

Comments are closed.