The House of Favourite Newspapers

Kama Unaikubali Simu Yako Ya tecno Kuna Dili Bomba Kwa Ajili Yako

xmass-campaign

Kampuni ya simu ya Tecno hii leo imezindua kampeni ya Christmas ambayo inawawezesha wateja wake kujishindia tiketi za safari ya kuzuru nchini Uingereza katika kampeni inayokwenda kwa jina la #KamaMbele. Uzinduzi huu ni katika jitihada za Tecno kuwapatia wateja wake zawadi katika msimu huu wa Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya na kuwawezesha kununua simu bora kwa gharama nafuu hivyo kuwawezesha kufurahia pamoja. Mwadada mrembo anayeng’arisha video za mastaa wa Bongo (Video Vixen), Hamisa Mobetto na Mshindi wa Big Brother Africa – Hotshots mwaka 2014, Idris Sultan ni mabalozi wa kampeni hii ambapo mmoja wao ( Idris au Hamisa) atashinda safari ya Uingereza akiambatana na shabiki mmoja.

Jinsi ya kushiriki ni kwamba mteja ataingia kwenye tovuti ya shindano ambayo ni http://tecnokamambele.co.tz/ atapiga kura kwa supastaa moja kati ya Idris au Hamisa kisha ataeleza kwanini anaikubali Tecno yake akitumia hashtag #KamaMbele na shabiki mshindi atapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na mashabiki katika hatua ya pili ya shindano. Mbali na kujishindia safari ya kwenda nchini Uingereza, wateja wa Tecno na Watanzania kwa ujumla wataweza kujishindia zawadi mbalimbali na kupata punguzo la bei katika simu za Tecno.

Tazama video hii na ingia http://tecnokamambele.co.tz/ kumpigia kura Idris Sultan uwe kwenye nafasi ya kuibuka mshindi wa Safari.

Endapo ungependa kusafiri na Hamisa Mobeto tazama video hii kisha ingia http://tecnokamambele.co.tz/ kumpigia kura.

Tembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kufahamu zaidi.

Facebook: https://www.facebook.com/TECNOMobileTanzania/

Instagram: https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/
Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ

Comments are closed.