The House of Favourite Newspapers

Kamanda MAMBOSASA Kazungumza haya kuelekea PASAKA – Video

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa limejipanga kuhakikisha wananchi wa Mkoa huo  wanasherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa utulivu na amani.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda Polisi wa Kanda Maaalum Dar, Lazaro Mambosasa amesema kuwa wananchi wa mkoa huo washerehekee Sikukuu hiyo kwa amani na utulivu kwani jeshi lake limejipanga vya kutosha na sehemu mbalimbali za ibada na fukwe zitaimarishwa kwa ulinzi ipasavyo kuhakikisha wananchi wanasherehekea na familia zao vyema.

 

Akizungumzia juu ya disko toto, Mambosasa amesema kuwa hajapata kibali chochote kutoka kwa watu wanaotaka kufanya hivyo kwa hiyo atakayeonekana akitoa burudani ya disco toto atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Mambosasa ameleza kuwa katika mzunguko wake wa kuhakikisha usalama unalindwa pia atatumia Helkopita kuzunguka mitaa mbalimbali ya jiji la Dar kwa ajili ya kuimarisha ulinzi zaidi.

 

Aidha, kuhusu uendeshaji wa vyombo vya moto dereva akiwa amelewa mambosasa amewaonya kutokuendesha ukiwa umezidisha kilevi na hivyo halitasita kuwachulia hatua wale wote watakaosababisha usumbufu na hata ajali.

MSIKIE MAMBOSASA AKIZUNGUKA

Comments are closed.