The House of Favourite Newspapers

Kamanda Ng’anzi, Shigongo Watoa Maagizo Makali Waliochoma Mabweni

0

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ramadhani Ng’anzi na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo, wamesema watu wote waliohusika kuchoma Mabweni ya Shule ya Sekondari Nyehunge watakasakwa hadi wapatikane.

 

Kauli hiyo imetolewa Septemba 30 mwaka huu walipotembelea Shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi walioathirika na janga la moto huo.


Aidha  Shigongo amewatoa hofu wanafunzi na walimu wa Shule hiyo kuwa watulie katika kipindi hiki kwani Ofisi ya mbunge kwa kushirikiana na serikali pamoja na wazazi watahakikisha  majengo yalioungua  yanarudi katika  hali nzuri kama ilivyokuwa awali.

 

Mabweni hayo yanayotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita ambayo yaliungua moto Septemba 27 na 29 mwaka huu ambapo magodoro na vifaa vingine vya  wanafunzi vimeungua moto.

 

” Niwaombe kuwa watulivu wakati huu ambao Serikali na ofisi ya mbunge inafuatilia suala hili kwa ukaribu sana na itakuja na mkakati wa kupambana na majanga haya ya moto” amesema Shigongo.

Matukio ya mabweni ya shule mbalimbali za sekondari nchi yamekuwa yakiteketea kwa moto na kuleta arhari kwa wanafunzi wa wanaosoma kwenye shule hizo.

 

Mkuu wa shule ya Nyehunge Sekondari Adofu Domisiani amesema wanafunzi usiku wa kuamakia leo wamelala wakiangalia TV baada kuwaomba walimu wao kufanya hivyo kutokana na hofu iliyotanda shuleni hapo, wanafunzi watakiwa kuwa watulivu kwa kipindi hiki ambacho wabweni yao yanachomwa moto.

Leave A Reply