The House of Favourite Newspapers

KAMANDA WA TRAFIKI AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUZUIA AJALI

Kamanda Musilimu akiongea kwenye hafla hiyo.

KAMANDA Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu, jana aliwaongoza waumini wa Msikiti wa Madinah uliopo Mbagala-Majimatitu eneo la Chasimba jijini Dar katika zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi la msikiti huo na kuwataka viongozi wa dini kukemea ulevi, ukorofi, visasi na na matendo mengine maovu kwa ajili ya kupunguza ajali za barabarani.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Musilimu  aliwashauri viongozi wa msikiti huo na viongozi wengine wa kidini,  wakiwemo viongozi wa makanisa,  kuwapa mawaidha na mahubiri mema waumini wao ili kudumisha amani na upendo.

Matukio katika picha Katibu wa msikiti wa Madina, Badi Bashiri,   akisoma historia fupi ya msikiti huo.

Imamu wa msikiti huo, Omary Masenga (kulia),  akimpa mkono, Alhaj Mzee Yusuf wakati akimkaribisha kwenye hafla hiyo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Shehe Twalib Bin Hamad,  akitoa mawaidha mbele ya umati uliokusanyika.

Kamanda Musilimu akichangia ujenzi wa msikiti huo kwenye harambee iliyoendeshwa kwenye hafla hiyo. Dua ikisomwa dakika chache kabla ya kuzindua jiwe la msingi la ujenzi huo.

Waumini wakikagua eneo ambalo msikiti unajengwa.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

Comments are closed.