Bagram: Watu wanne wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa baada ya Wanamgambo wa Taliban kuishambulia Kambi Kubwa ya Jeshi la Marekani ya Bagram nchini Afghanistan.
Jeshi linaloongozwa na NATO, limesema kuwa shambulizi hilo ni la kujitoa muhanga kwani mlipuaji huyo alivalia bomu bila wao kujua aliwadanganya kuwa nyeye ni miongoni mwa wafanyakazi wa kambi hiyo, wakati wafanyakazi walipokuwa wakiwasili katika kambi hiyo kwa shughuli za siku.
Kundi la Taliban linasema kuwa ndilo lilihusika. Hakuna taarifa zaidi kuhusu uraia wa wale waliouawa.
Comments are closed.