The House of Favourite Newspapers

KANGI LUGOLA APONGEZA MASHABIKI, KUJITOKEZA SIMBA DAY

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akisalimiana na Kaimu Rais wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’.
…Lugola akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Klabu ya Simba kabla ya kuanza kwa mchezo wao dhidi ya Asante Kotoko katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mwibara-Bunda ambaye pia amemwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza Klabu ya Timu ya Simba na mashabiki wake kwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha lao lijulikanalo kama ‘Simba Day’.

Katika hafla hiyo zaidi ya mashabiki elfu 58 wameingia uwanjani ikilinganisha na mashabiki wa mwaka jana walioingia elfu 42.

Mbali na Kangi Lugola pia Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amehudhuria hafla hiyo.

Comments are closed.