The House of Favourite Newspapers

BILLION 32.2 ALIZOTUMIA KANYE WEST KUMNUNULIA MKE WAKE ZAWADI YA KRISMAS

 

Rapa Kanye West amemnunulia mke wake Kim Kardashian ghorofa kubwa la kifahari lililopo Miami Beach kwa dola za kimarekani Milioni 14 (Tsh.Bilion 32.2)

 

Jengo hilo lina futi za mraba zipatazo 4,700 ambalo ndani kuna sehemu ya mazoezi ya binafsi, mgahawa mdogo na sehemu ya kuegesha magari kwa chini.

 

Chanzo cha karibu na wawili hao kimeeleza kwamba, Kim na Kanye mwezi uliopita walionekana wakiangalia mjengo huo na wakawa kwenye mkakati wa kulinunua kwa dola milioni 14.

 

Mwaka 2016 mwenye jengo hilo, Alan Faena aliliambia jarida la New York  kwamba jengo hilo limedizainiwa kwa namba nzuri na ya kupendeza ikiwemo mgahawa wa nyota 5, sehemu kubwa ya Art (sanaa) na sehemu nyinginezo.

 

Ripoti nyingi zinasema kwamba hiyo ni zawadi ya Kanye West kwa mke wake Kim Kardashian.

Comments are closed.