The House of Favourite Newspapers

KASEKE APEWA MWAKA YANGA

 

Deus Kaseke

UNAAMBIWA hivi ile ishu ya Deus Kaseke kwamba anakwenda Sauzi ni geresha tu, kama mambo yatakwenda sawa basi leo Jumamosi kiungo huyo wa Singida United, anasaini mkataba wa mwaka mmoja Jangwani.

 

Kaseke ambaye alichezea Yanga msimu miwili iliyopita kabla ya msimu wa 2017/18 kujiunga na Singida United. Chanzo makini kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa Kaseke ilikuwa asaini mkataba jana Ijumaa lakini kuna vitu vikashindikana katika makubaliano yao hivyo leo Jumamosi anatarajia kusaini kandarasi yake.

 

Kiliongeza kuwa Kaseke alikuwa anaidai Singida fedha yake ya usajili uliopita hivyo Yanga wameingilia na sasa watamlipa fedha anayoidai kutoka singida kisha watamungozea kiasi kingine ili asaini mkataba haraka.

 

Pia Yanga ililazimika kumzuia nyota huyo kucheza mechi ya jana ya Kombe la Kagame dhidi ya APR ya Rwanda kwa hofu ataumia hivyo kushindwa kumtumia kwenye michuano yake ya kimataifa ambapo wanashiriki Kombe la Shirikisho.

 

Alipotafutwa Kaseka alisema: “Nipo kwenye mazungumzo na Yanga na yanakwenda vizuri muda wowote nitasaini mkataba.” Awali baada ya Kocha Hans Pluijm kuondoka Singida na kujiunga na Azam FC, Kaseke ilidaiwa kwamba hajaongeza mkataba atakwenda Afrika Kusini.

Comments are closed.