The House of Favourite Newspapers

KATIBU MKUU CCM AWAJIBU UBALOZI WA MAREKANI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bashiru Ally.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bashiru Ally,  ametoa msimamo wa chama hicho kuhusu taarifa iiliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini kuhusu uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu  na kata 71 uliofanyika hivi karibuni.

 

Baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao CCM imepata ushindi mkubwa, Ubalozi wa Marekani waliamua kutoa taarifa kwa vyombo vya habari wakionesha kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo.

 

Katibu huyo amesema ameisoma na kuilewa taarifa hiyo na kwamba  chama chake kinazingatia zaidi uhuru wa kitaifa na wanayo dhama ya kuulinda.

 

“Kauli ambayo wameitoa inagusa maeneo mengi na matarajio yangu taasisi zote zinazohusika zitazingatia madukuduku yao.

 

“Ninachojua mimi chaguzi hizi zimefanyika kwa misingi ya kisheria na mataifa mengine likiwamo la Marekani wanapaswa kuheshimu chaguzi zetu,” amesema Dk.Bashiru Ally.

 

Mbali ya kauli hiyo,  wachambuzi waliobobea kwenye medani za siasa nchini akiwamo Dk. Benson Banna,  wamesikitishwa na taarifa hiyo ya ubalozi wa Marekani.

Comments are closed.