The House of Favourite Newspapers

Kauli ya Kalanga Baada ya Kuibuka Mshindi Monduli – Video

IKIWA ni muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiro cha ubunge jimbo la Monduli, mbunge mteule Julius Kalanga (CCM), amewashukuru wananchi wote waliompigia kura na kumpa ushindi huo, huku akiahidi kuyafanyia kazi mambo yote ya msingi waliyokubaliana wakati wa kampeni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kalanga amesema kuna mambo mengi atakayoyatekeleza lakini vipaumbele vyake kwanza ni maji ambapo amesema atahakikisha anashirikiana na serikali ili kuhakikisha jimbo hilo linapatiwa maji ya uhakika na kuondoa kero ambayo ni ya muda mrefu kwa wananchi hao.

Aidha suala la migogoro ya ardhi,ni miongoni mwa mambo yanayowasumbua wananchi kwani wamekuwa wakipata tabu kutokana na kugombania ardhi,hivyo atawasaidia kubainisha mipaka na kuwafanya wananchi wafanye shughuli zao pasipo kuwa na muingiliano.

Kuhusu afya, Kalanga amesema,maeneo mengi katika jimbo hilo hakuna vituo vya afya ambapo vituo vingi vipo umbali mrefu,atahakikisha kila kijiji kinakuwa na kituo cha afya ili kuepusha vifo vya akina mama na watoto vinavyotokana na akina mama kijufungulia nyumbani.

Kalanga ataliongoza jimbo la Monduli kwa kipindi cha miaka miwili (2) iliyosalia, baada ya kufanyika uchaguzi wa marudio 16, September 2018, kutokana na kujivua uanachama kutoka Chadema na kuhamia ccm,na hatimaye kupata ushindi kwa asilimia 95%.

VIDEO: MSIKIE KALANGA AKIFUNGUKA

Comments are closed.