The House of Favourite Newspapers

Keissy: Sijaoga Siku Tatu, Wizarani Kuna ‘Ujambazi’ – Video

MBUNGE wa Nkasi, Ally Keissy, akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, amefunguka na kudai kuna ubadhirifu mkubwa katika miradi ya maji inayojengwa Mkoa wa Rukwa huku akimtaka Spika kuunda tume maalum kwa ajili ya kukagua miradi hiyo na kuanika wizi unaofanyika.

 

Keissy ameyasema hayo leo Jumatano Bungeni Mjini Dodoma na kudai kuwa baada ya kuibua ubadhirifu huo baadhi ya miradi imesimamishwa huku wananchi wakiteseka kwa kukosa maji na kuongeza kuwa kutokana na hali hiyo, imefikia hatua amemaliza siku tatu bila kuoga.

 

Aidha, Keissy amedai katika wizara hiyo, inaonekana kuna ‘ujambazi mkubwa’ (wizi wa pesa za miradi ya  maji) ambayo inatokana na jasho la wananchi kupitia kodi zao huku akiwataka wasimamizi wa miradi hiyo kufanya kazi kwa manufaa ya taifa na si kwa ajili ya matumbo yao.

“Mradi wa Kamwanda Kilando umeingiwa mkataba wa Tsh 7.7 bilioni na Mkandarasi Wimbe mara kumi ya uwezo wake ambao ni Shilingi milioni 7.5. Baraza la madiwani Nkasi walimkataa hana sifa, lakini amepewa mradi huo kindugu. Mwaka jana huyu mkandarasi alikula hela, na tenda yake haikutangazwa. Nkasi hakuna hata mradi mmoja unaotoa maji.

 

“Zaidi ya bilioni tatu ni wizi, miradi yote ya Rukwa ni wizi, Rais anakusanya pesa, idara ya maji zinapita tu, mimi mbunge nimekaa siku tatu sijaoga. Sikusomea uhandisi lakini huwezi kunidanganya,” alisema Keissy.

 

MSIKIE KEISSY AKIFUNGUKA

Comments are closed.