The House of Favourite Newspapers

Kesi ya ‘Malkia wa Meno ya Tembo’ Kusikiliza Mashahidi

malkia-3

DAR ES SALAAM: Kesi inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan (66) mamarufu kama Malkia wa Meno ya Tembo na wenzake leo imeahirishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Kisutu kutokana na wakili wa serikali, Faraja Nchimbi,  kuiambia mahakama kuwa haikupeleka mashahidi kwani alitambua kuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, anayesikiliza kesi hiyo  bado yupo likizo.

Aidha watuhumiwa wamerudishwa rumande baada ya  hakimu kukubaliana na ombi hilo lakini akamtaka wakili huyo kuhakikisha siku hiyo iliyopangwa anapeleka mashahidi wake, hivyo kesi hiyo ikapangwa kusikilizwa Februari 3, mwaka huu.

malkia-2

Yang Feng Glan, maarufu kama Malkia wa Meno ya Tembo (wa pili kushoto, mwenye miwani) alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo.

Naye wakili wa upande wa utetezi, Masumbuko Lamwai,  aliiambia mahakama kuwa sasa mwaka mmoja kesi hiyo inapigwa tarehe kwa sababu ya  kukosekana mashahidi wa upande wa jamhuri na mteja wake anazidi kukaa rumande.  Alisema bora angelikuwa nje kwa dhamana kuliko kuendelea kuwa rumande na akaiomba mahakama kutokukubali kusikiliza sababu zinazotolewa na wakili wa jamhuri kwa sababu zisizokuwa za msingi.

Glan maarufu kwa jina la ‘Malkia wa Meno ya Tembo’ anashtakiwa na mfanyabiashara Salvius  Matembo (39) na Manase Philemon (39).

malkia-1Awali baada ya hati ya mashtaka kuwasilishwa, washtakiwa walisomewa mashtaka ambayo waliyakana. Upande wa mashtaka unaodai upelelezi umekamilika ulisema kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014 watu hao  walijihusisha na biashara ya nyara za serikali bila kibali.

Katika kipindi hicho wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1,889 zenye thamani ya Sh bilioni 5.4 bila leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori.

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.