The House of Favourite Newspapers

Kidoa Afungukia Rushwa ya Ngono… “Nay wa Mitego Alinilipa” – Video

Hii ni sehemu ya kwanza ya mahojiano ya muuza nyago kwenye video za wasanii, Kidoa Salum, mrembo wa Uswazi hadi kuwa staa. Kupitia Exclusive Interview ya GLOBAL TV ONLINE, Kidoa anayaelezea maisha yake ya sanaa na vikwazo alivyopitia mpaka kutusua.

 

“Nilikuwa nikifanya video vixen ili watu wanijue na nipate connection, lakini lengo langu ilikuwa nije kuwa mwigizaji mkubwa hapa nchini. Baada ya kufanikisha hilo nikapata Tamhtilia ya HUBA ninayocheza sasa hivi, nimeuwa bize na kazi yangu.

 

“Changamoto kubwa nimezipitia ikiwemo ni vishawishi vya rushwa ya ngono ili wanisaidie. Kwa sasabu mimi ni mtoto wa kike ninaziona ni za kawaida na nakaribiana nazo tu. Video vixen hailipi kabisa, watu wanafanya tu ili kujulikana. Mara nyini utapewa pesa ya nauli tu.

 

“Nashukuru nilifanya kazi na NAY WA MITEGO katika video yake ya AKADUMBA, Nay alinilipa japo haikuwa kivile, lakini kwa wakati ule ilikuwa inatosha. Watu wengi husema mimi nilitoka kimapenzi na Nay ili anipe kazi, hili suala nitaendelea kuliongelea siku zote, sijawahi kutoka kimapenzi na Nay wa Mitego.

 

‘Imezoeleka kwamba huwezi kufanya kazi ya vixen bila kutoa penzi, kwangu mimi haikua hivyo, labda kwa sababu Nay ni mshikaji wangu sana, nilifanya kazi nikalipwa basi kila mmoja akaendelea na shughuli zake.

 

“Kuna kipindi nilipata bwana akaninunulia gari, akaniahidi kunioa, lakini kadri siku zilivyokuwa zinakwenda mwaka miaka miwili nikaona kabisa hatimizi malengo yake, nikaamua kuachana nae na ku-focus kwenye kazi yangu.

MSIKILIZE KIDOA

Comments are closed.