The House of Favourite Newspapers

KIFO CHA MASOGANGE CHAMRUDISHA NYUMBANI MWANAMITINDO WA KIMATAIFA

Mbutananga (kulia) akikata keki.
Akimlisha keki mmoja wa wageni waalikwa.

Mwanamitindo wa kimataifa ambaye ni Mtanzania anayeishi nchini Uingereza, Flora Lymo maarufu kwa jina la Mbutananga, ametua nchini baada ya kupata taarifa za kifo cha Agnes Gerald Masogange ambaye amesema alikuwa ni kama mdogo wake.

Mwanamitindo huyo ndiye hivi karibuni alimvalisha Zarinnah Hassan ‘Boss Lady’ nchini Uingereza. Mbutananga amesema sambamba na Zari anatamani pia kufanya kazi na  mastaa mbalimbali wa Bongo akiwemo msanii wa Bongo Muvi, Wema Sepetu.

Akifurahia jambo na Eshe Buheti.
Msanii wa filamu Eshe Buheti akifungua shampeni.
Hii ndiyo keki yenyewe ikiwa muundo boti.
Sehemu ya bufee, Vipapatio vya kuku vilikuwa vya kumwaga.

Mbutananga amesema tukio la kifo cha Masogange limekaribiana na siku yake ya kuzaliwa hivyo aliamua kufunga safari kutoka Uingereza kuja nchini kuhudhuria msiba huo pamoja na kufanya sherehe yake ya kuzaliwa ambayo aliifanya jana jioni kwenye Hoteli ya Giraffe iliyopo Mbezi Beach jijini.

 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS GPL

Comments are closed.