The House of Favourite Newspapers

KIJANA ANAYETUNUKU PENZI VIBIBI!

Kijana Kyle na kibibi Marjorie wakiwa katika hisia za kimapenzi.

Wakiwa katika pozi la kamera.
Mama yake Kyle, aitwaye Cecilia Jones (kulia) akiwa na Marjorie.
Kyle akiwa na mpenzi mwingine mwenye umri wa miaka 64.

KIJANA Kyle Jones (31) ana tabia isiyo ya kawaida. Yeye hupenda marafiki wa kike wenye umri mkubwa kuliko yeye. Hivi sasa marafiki zake hao wa kike ambao ni watano, wote wana umri zaidi ya miaka 60. Na mpenzi wake mkuu kati ya hao anaitwa Marjorie McCool aliye na umri wa miaka 91, ikimaanisha anamzidi kijana huyo kwa miaka 60!

 

Kyle alianza mahusiano ya mapenzi kwa mara ya kwanza na mwanamke aliyekuwa na umri wa miaka 50 wakati huyo yeye akiwa na umri wa miaka 18. Anasema yeye huvutiwa na wanawake wazee na kwamba anaridhika kabisa katika suala la mapenzi na huvipeleka vibibi hivyo nyumbani kwao kumwonyesha mama yake aitwaye Cecelia Jones ambaye naye amekubaliana naye.

 

Akiwa ni kijana mwenye umbo na sura ya kuvutia, mkazi huyo wa Augusta, Georgia, Marekani, anasema: “Kila mtu na akili yake, wengine wanapenda wanawake vijana, warefu, wembamba, wenye nywele za aina mbalimbali, mimi napenda wanawake wazee.

 

“Kila ninapomtongoza mwanamke mzee, kitu cha kwanza kuniambia ni kwamba mimi mdogo mno. Hilo hunifurahisha na mimi huwaambia kwamba wakinikubali watafaidi.”

 

Mara ya kwanza kukuatana na bibi Marge – ambacho ni kifupi cha Marjorie – ni kwenye duka la vitabu ambapo alimwomba namba yake na kibibi huyo, aliyekuwa anaishi pekee kwa miaka 37 baada ya kuachana na baba wa watoto wake sita — alimpatia na kukubali kukutana naye.

 

“Mwanzoni nilikuwa naona wivu kwa wanawake wengine, lakini kila mara alikuwa akija kwangu akisema mimi ndiyo bora zaidi. Hadi sasa tunapendana sana. Huwa ninavaa nguo za kuvutia kimapenzi kitandani. Huwa sivui sidiria yangu, kwani hakuna kilichobakia.

 

“Familia yangu ina wanaume wengi zaidi na hawajali ninachofanya. Umri wao ni miaka 71, 63, 61, 52 na 50. Watu wanapotuona wanafikiri huyo ni mwanangu, au hata mjukuu, kwani ninao wajukuu wakubwa kuliko yeye,” anasema kibibi huyo.

 

Pamoja na vibibi anavyovifuata kutoamini kwamba anavipenda, Kyle anasema anavipenda na kwamba anapenda makunyanzi yao na matiti yao ya kawaida yaliyochoka kwani ni vitu vya asili, na akasisitiza kwamba hapendi watu wanaojibadilisha sura kwa kufanya operesheni.

 

“Watu huniambia navipenda vibibi hivyo kwa kutegemea urithi au kununuliwa vitu,” anasema Kyle akisisitiza kwamba anawapenda wanawake hao na wao wanampenda.

 

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA

Comments are closed.