The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kijana wa Miaka 22 Atiwa Nguvuni kwenye Mauaji ya Copenhagen, Denmark

0
Raia wa Denmark wakikimbia kuokoa uhai wao kufuatia shambulio la risasi katika Jumba la Biashara jijini Copenhagen

 

IMEBAINIKA kuwa kijana mwenye umri wa miaka 22, ametiwa nguvuni baada ya kubainika kuwa ndiye mhusika wa shambulio la jumba la kibiashara jijini Copenhagen nchini Denmark ambapo ripoti zinadai kuwa jumla ya watu 3 wameuawa katika shambulio hilo.

 

Inspekta wa Polisi, Soren Thomassen amewaambia waandishi wa habari kuwa kijana wa miaka 22 alikamatwa na polisi na tayari anashtakiwa kwa makosa ya mauaji.

 

Amebainisha kuwa hakukuwa na ishara nyingine kama kuna uwezekano wa kuwepo kwa mtu mwingine aliyeshiriki katika shambulio hilo ingawa pia amebainisha kuwa ni vigumu kwa sasa kujua sababu hasa ilikuwa ni ipi ya utekelezaji wa shambulio hilo.

 

Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen

Naye waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen alitoa kauli siku ya Jumapili akisema:

 

“Denmark ilikumbwa na shambulio la kikatili ambapo watu kadhaa waliuawa na wengi wao wakijeruhiwa wakiwemo watoto wasiokuwa na hatia, vijana pamoja na wazee wate hao walidhurika.”

 

Aliendelea kwa kusisitiza kuwa mji mzuri na ambao umekuwa salama kwa muda wote ulibadilishwa ndani ya sekunde moja hivyo ametoa wito kwa raia wote wa Denmark kuwa pamoja na kushirikiana katika wakati huu mgumu.

 

Vyombo mbalimbali vya habari nchini Denmark vilichapisha picha kuonesha maafisa wa serikali wakiwa katika eneo la tukio huku raia wakikimbia hovyo na wengine wakijificha ndani ya jumba la biashara ili kuokoa uhai wao.

Leave A Reply